Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Historia

  • Bonde la Kati lilianzishwa rasmi tarehe 29 Oktoba, 2004 likiwa kati ya mabonde tisa yaliyopo nchini kwa mujibu wa Sheria Namba 42 ya mwaka 1974 na kufanyiwa marekebisho na Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya mwaka 2009.

  • Bonde la Kati ni la tatu kwa ukubwa Baada ya Rufiji na Ziwa Tanganyika, likiwa na ukubwa wa kilometa za mraba 163,600. Bonde hili ni shirikishi, ambapo asilimia 88 ya eneo lake liko upande wa Tanzania na asilimia 11.5 lipo upande wa Kenya.

  • Bonde la kati lina mabonde madogo-madogo tisa ambayo ni; Bonde Dogo la Ziwa Eyasi, Bonde Dogo la Ziwa Manyara, Bonde Dogo la Ziwa Natroni, Bonde Dogo la Bubu, Bonde Dogo la Nyanda za Masai, Bonde Dogo la Monduli A, Bonde Dogo la Monduli B, Bonde Dogo la Namanga na Bonde Dogo la Olduvai