Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Faida za kuwa na kibali cha matumizi ya maji



a). Kukusaidia kupata mkopo kwa urahisi



b). wenye kibali ana uwezo wa kusikilizwa mbele za vyombo vya sheria endapo mtu, mamlaka au taasisi watamwingilia katika matumizi ya kibali chake

c). Kibali kinawawezesha bodi ya maji ya bonde kufahamu kiasi cha maji kilichotolewa katika chanzo cha maji na hivyo kulinda haki ya wale wenye vibali

d). Kibali kinampa uwezo mmiliki kupinga muombaji mwingine anayeweza kumuathiri kutumia maji

Mwenye kibali anauwezo wa kujiunga na wengine katika chanzo hicho kuunda chombo cha watumia maji.

e). Vibali vya kutumia maji vinasaidia katika kutatua au kuepuka migogoro mbalimbali ya kugombania maji kwa watumiaji mbalimbali.

Kuwa na kibali cha matumizi ya maji kinakupa uhalali wa kutumia maji kisheria pia endapo kutatokea mgogoro kati ya mtu am,baye hana kibali mwenye kibali kisheria atapewa kipaumbele cha kusikilizwa.