Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Habari

UJENZI WA BWAWA LA SOITSAMBU WILAYANI NGORONGORO UMEKAMILIKA ASILIMIA 100%, MAMBO MAZURI YANAKUJA KWA WANANCHI


UJENZI WA BWAWA LA SOITSAMBU WILAYANI NGORONGORO UMEKAMILIKA ASILIMIA 100%, MAMBO MAZURI YANAKUJA KWA WANANCHI

Mradi wa ujenzi wa bwawa Soitsambu wilayani Ngorongoro mkoani Arusha umekamilika asilimia 100% ya utekelezaji na unatarajiwa kuwanufaisha wananchi zaidi ya 5106 katika vijiji mbalimbali pamoja na mifugo 31943 hadi kufikia mwaka 2042

Bwawa hilo lilijengwa na wizara ya maji kupitia Bodi ya Maji Bonde la Kati.

Hii inakwenda sambamba na juhudi za serikali za kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya vijijini kufikia asilimia 85% ifikapo mwaka 2025 ambapo mradi huu ni moja ya miradi mingi mikubwa hapa nchini ambayo inakuja kuwa na matokeo ya moja kwa moja kwa wananchi wanaolizunguka bwawa hilo.

Bwawa hilo litakuwa na ukubwa wa kubeba maji yenye lita za ujazo milioni 14.3 na litaleta maendeleo kwa wananchi kwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa vijijini.

Mradi huu ulianza utekelezaji wake mwezi Juni na kukamilika mwezi wa Nane 2025.
#Utunzaji wa vyanzo vya maji ni jukumu letu sote

Imetolewa na;
Kitengo cha Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano
Bodi ya Maji Bonde la Kati