Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Habari

MAFUNZO YA BODI YA SABA YA BODI YA MAJI BONDE LA KATI


Kiongozi mstaafu aliyekuwa Afisa wa Maji Bonde la Rufiji  William  Mwaluvande ametoa mafunzo Tarehe 19/2/2026 katika ofisi kuu ya Bodi ya Maji Bonde la Kati mjini Singida.

Lengo la mafunzo hayo ni kuipa nguvu, utashi, mbinu, pamoja na uwelewa wa uwajibikaji wa Bodi ya Maji Bonde la Kati katika majukumu ndani ya bodi.
 
Pia mwaluvande alisema lugha nzuri, pamoja na kujitoa kikamilifu katika majukumu ni mbinu sahihi ya kuleta maendeleo ndani ya Bodi.
 
Pamoja na kusema hayo aliwataka viongozi wa Bodi  kuwapa elimu endelevu  watumishi wao pamoja na kuwajengea mawasiliano mazuri na watu wengine  kwani hii itawapa uwezo mzuri  katika kazi zao za kila siku.