Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Habari

MENEJIMENTI YA IDBWB YAKUTANA NA (N&S)


Singida 29/5/2026.Menejimenti ya Bodi ya Maji Bonde la Kati yazungumza na N&S. 

Menejimenti ya Bodi ya Maji Bonde la Kati ikiongozwa na Mhandisi Danford Samson (Mkurugezi-IDBWB)wakwanza kushoto, imekutana na mkandarasi N&S (Subs Contractor)wakwanza kulia ,Mwamkoko. Mkandarasi huyu anaiwakilisha kampuni ya GDS HYDRO AND CIVIL ENGINEER CO.LIMITED inayotekeleza Mradi wa uchimbaji wa visima katika eneo la Mwamkoko ndani ya Manispaa ya Singida. 
Lengo la Menejimenti kukutana na mkandarasi huyu ni kutaka kujua maendeleo na changamoto ya Mradi wa uchimbaji wa visima unaoendelea hadi sasa. 

Pia uchimbaji huu ni moja ya utekelezaji wa upatikanaji wa maji endelevu na ya uhakika chini ya Mradi wa miji 28 na kutokomeza changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama ndani ya Manispaa ya Singida.