Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Majukumu

1. Kusimamia na kuratibu hifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji

2. Kuratibu mipango ya matumizi ya maji katika Bonde

3. Kukusanya na kutunza takwimu za mitiririko na hali ya maji kwenye rasilimali za maji

4. Kugawa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya uchumi na ya jamii.

5. Kuhakikisha maji yanagawiwa kwa uangalifu kwa kuzingatia mahitaji ya mazingira.

6. Kusimamia na kutatua migogoro inayotokea katika matumizi ya maji.

7. Kutoa tahadhali mapema kuhusu majanga ya asili kama vile mafuriko, ukame,uchafuzi wa maji unatokana na matumizi mabaya ya kemikali na uchafuzi mwingine toka viwandani.

8. Kuwafikisha mahakamani wanavunja sheria au kukiuka taratibu zilizowekwa kuhusu matumizi, ulinzi na uhifadhi wa vyanzo vya maji.