Habari
UJENZI WA BWAWA LA GIDAHABABIEG WILAYANI HANANG UMEFIKIA ASILIMIA 80%, NA MAMBO MAZURI YANAKUJA KWA WANANCHI

UJENZI WA BWAWA LA GIDAHABABIEG WILAYANI HANANG UMEFIKIA ASILIMIA 80%, NA MAMBO MAZURI YANAKUJA KWA WANANCHI
Mradi wa ujenzi wa bwawa Gidahababieg wilayani Hanang mkoani Manyara umefikia asilimia 80% ya utekelezaji na unatarajiwa kuwanufaisha wananchi zaidi ya 9,254 wa vijiji (5) na mifugo ipatayo 11,451.
Bwawa hilo linajengwa na wizara ya maji kupitia Bodi ya Maji Bonde la Kati.
Hii inakwenda sambamba na juhudi za serikali za kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya vijijini kufikia asilimia 85% ifikapo mwaka 2025 ambapo mradi huu ni moja ya miradi mingi mikubwa hapa nchini ambayo inakuja kuwa na matokeo ya moja kwa moja kwa wananchi wanaolizunguka bwawa hilo.
Bwawa hilo litakuwa na ukubwa wa kubeba maji yenye lita za ujazo 602,015,000 na litakapokamilika litanufaisha kuleta maendeleo kwa wananchi kwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa vijiji.
Mradi huu ulianza utekelezaji wake 15/06/025 na bado unaendelea.
#Utunzaji wa vyanzo vya maji ni jukumu letu sote
Imetolewa na;
Kitengo cha Tekinologia ya Habari na Mawasiliano
Bodi ya Maji Bonde la Kati