Habari
Wataalamu wa Bodi ya Maji Bonde la Kati wakiongozwa na Mkurugenzi Eng. Danford Samson wamewapitisha wenzao kutoka Zanzibar kuhusu usimamizi na utunzaji wa vyanzo vya maji.

Wataalamu wa Bodi ya Maji Bonde la Kati wakiongozwa na Mkurugenzi Eng. Danford Samson wamewapitisha wenzao kutoka Zanzibar kuhusu usimamizi na utunzaji wa vyanzo vya maji.
Wataalamu hao wanatoka Wizara ya Maji,Nishati na Madini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mafunzo yamefanyika katika ofisi za Bodi ya Maji Bonde la Kati zilizopo Singida Mjini.
Lengo la mafunzo ni kujenga uelewa kuhusu namna sahihi ya kufanya utunzaji na usimamizi wa rasilimali za maji zinavyofanywa na Mabonde nchini.