Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Habari

UTAFITI WA MAJI CHINI YA ARDHI WILAYANI MONDULI


Kazi ya utafiti wa maji chini ya Ardhi kupitia programu ya kuvipatia vijiji vyote maji Nchini kwa kuchimba Kila jimbo Visima vitano, imeendelea wilayani Monduli Mkoani Arusha ambapo jumla ya vijiji vitano vimefanyiwa utafiti wa maji chini ya Ardhi kwa ajili ya uchimbaji wa visima virefu. Katika hatua hiyo wananchi wa jimbo la Monduli wameishukuru na kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi na hatua mbalimbal inazochukua katika kuhakikisha wanapatiwa maji safi na Salama.