Habari
JUMUIYA YA WATUMIA MAJI BWAWA LA MWAMAPULI YATEMBELEA OFISI ZA BODI YA MAJI BONDE LA KATI

Viongozi wa Jumuiya ya Watumia Maji Bwawa la Mwamapuli Wametembelea Ofisi za Bodi ya Maji Bonde la Kati kwa Lengo la kufahamu Ofisi za Bodi ya Maji Bonde la Kati zilipo, Kufahamiana na Watumishi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Kuleta Taarifa zao za Utekelezaji, lakini piah wakaona ni Busara Kushukuru Bodi ya Maji Bonde la Kati kwa kuwapa Mradi wa Ufugaji Nyuki ambapo kwa juhudi zao na kujituma kwao ndani ya mwezi mmoja wamefanikiwa kutundika mizinga ya nyuki na nyuki tayari wapo kwenye mizinga yao na walipoona kwamba ni mradi ambao wameupenda wakaona waje ofisi za Bodi ya Maji Bonde la Kati kushukuru kwa kuwa ni jambo jema walilolifanya Bodi ya Maji Bonde la Kati inaasa Jumuiya Zingine ziweze kuiga mfano huu kwa utekelezaji wa utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji