Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Habari

MKUU wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude,amezindua zoezi la uwekaji alama kwenye mipaka ya vyanzo vya maji katika Mabwawa ya Songwa na Mhumbu wilayani humo ili kuvilinda vyanzo hivyo vya maji kwa kuzuia shughuli za kibinadamu.

Zoezi hilo la limefanyika jana pamoja na upandaji miti, kwa kuratibiwa na Bodi ya Maji Bonde la Kati.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya kuzindua uwekaji wa alama hizo, Mhandisi wa Mazingira kutoka Bodi ya Maji Bonde la Kati, Nyacheli Mramba, alisema wameweka Alama hizo za mipaka na Mabango ili kuzuia wananchi wasifanye shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo hivyo ili kuvilinda visitoweke.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude, ametoa wito kwa wananchi wasifanye shughuli za kibinadamu kwenye Mabwawa hayo, ikiwamo na kufanya shughuli za kilimo na uchimbaji madini, bali wavitunze vyanzo hivyo vya maji kwa faida yao na vizazi vijavyo.

“Natoa wito kwa wananchi vitunzeni vyanzo hivi vya maji msifanye kabisa shughuli za kibinadamu, na katika Mabwawa haya yamejengwa Matangi kwa ajili ya kunyweshea mifugo yatumieni na msiingize tena mifugo ndani ya maji,”amesema Mkude.