Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Habari

MH, WAZIRI WA MAJI JUMAA AWESO AKIKAGUA BWAWA LA NANJA


Wataalam kutoka Bodi ya maji Bonde la kati walifika katika bwawa la Nanja lililopo katika Wilaya ya Monduli kwa lengo la kukagua. Bwawa hilo ndiyo tegemeo kubwa kwa wakazi wa vijiji 30 kama chanzo cha maji pekee baada ya kumeguka kingo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Mheshimiwa Waziri Maji Jumaa Aweso alifika kukagua athari zilizojitokeza kutokana na bwawa kumeguka

Mheshimiwa Waziri Maji Jumaa Aweso alizungumza na wananchi wa Kata za Lepruko, Sepeko, na Makuyuni. Waziri wa maji alitoa Maelekezo kwa Wataalamu wa Wizara kama ifuatavyo kwanza kutumia taaluma zao kuhakikisha Bwawa hilo linakarabatiwa kwa dharula haraka kuanzia kesho tarehe 19.04.2024 kudhibiti maji kuendelea kupotea pili kufanya usanifu wa kina nyakati za kiangazi kusudi bwawa hilo liweze kukarabatiwa kwa uhakika zaidi.