Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Habari

MAADHIMISHO YA MIAKA 63 YA UHURU WA TANZANIA BARA


Katika Maadhimisho ya Miaka 63 ya Kumbukumbu ya Uhuru wa Tanzania Bara yenye kauli Mbiu "UONGOZI MADHUBUTI NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI NI MSINGI WA MAENDELEO YETU.", Bodi ya Maji Bonde la Kati imeshiriki katika zoezi la Upandaji Miti 551 lililofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Mandewa.

Zoezi hilo la Upandaji wa miti 551 liliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa singida Mhe. Halima Dendego, katika Maadhimisho hayo ya Miaka 63 ya Uhuru Mhe. Halima Dendego alitumia nafasi hiyo kutembelea wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ili kuwapatia faraja.