Habari
KIKAO CHA TATU CHA BODI YA SITA

Leo 30/09/2023
KIKAO CHA TATU CHA BODI YA SITA KIMEFANYIKA KATIKA UKUMBI WA BODI YA MAJI BONDE LA KATI-SINGIDA.
Katika kikao hicho kilijadili Taarifa ya Utekelezaji wa Shughuli za Bodi ya Maji Bonde la Kati katika Kipindi cha Julai-Septemba, 2023. Katika Taarifa hiyo ya Utekelezaji Kazi zilizotekelezwa ni kama ifuatavyo
1.Elimu ua utunzaji na uhifadhi wa rasilimali za maji ilitolewa kwa wananchi wa kata ya Endagaw Wilaya ya Hanang na Mang'ola Wilaya ya Karatu.
2.Mafunzo ya kujenga uwezo yalitolewa kwa Jumuiya 10 za watumia maji ambazo ni;Mto wa Mbu, Ngarenanyuki, Eyasi, Endagaw, Ziwa Bassotu, Mwamapuli, Kiru-Magugu, Kisangaji-Magara, Songwa na Mhumbu
3.Ukarabati wa bwawa la Enguikumenti unaendelea na kazi imekamilika kwa asilimia 85
4.Ukarabati wa bwawa la Mwalukwa Wilayani Shinyanga unaendelea na kazi imekamilika kwa asilimia 80
5.Ukarabati wa mabwawa mawili ya Ngofila na Kilileli Wilayani Kishapu inaendelea na mitambo imeanza kwenda kwenye eneo la ujenzi.
6.Ujenzi wa mabwawa madogo Wilayani Bahi(Mpamantwa na Uhelela) umeanza na umefikia asilimia 90 kwa bwawa la Uhelela na 5% kwa bwawa la Mpamantwa
7.Ujenzi wa bwawa la kuzuia mchanga katika kijiji cha Qang'dend Wlayani karatu na utekelezaji wake umekamilika kwa asilimia 95%
8.utafiti wa maji chini ya ardhi umefanyika katika vijiji vya Wilaya za babati, Singida, chemba, Iramba na Mbulu ambapo maeneo 51 yaliotafitiwa 16yalipendekezwa kwa uchimbaji wa visima
9.Utafiti wa Maji juu ya ardhi Umwfanyika katika Wilaya za Babati na Mbulu Katika mito ya Hainu-Quamquam, Magara-Datlaa, Tsoray na Qamey
10.Vituo 11 vya kukusanyia takwimu za hali ya hewa vimekarabatiwa na 2 vya kukusanyia takwimu za mvua vimekarabatiwa
11.Jumla ya maombi 07 ya vibali yamepokelewa na yamesajiliwa kwenye daftari la maombi ya vibali, Maombi 21 yanasubiria maoni kutoka kwa wadau
12.Ukusanyaji wa takwimu za maji chini ya ardhi umefanyika kwenye visima vya ufuatiliaji mwenendo wa maji chini ya ardhi.Takwimu zimekusanywa kwenye vituo vya Sindida yard, olmolog, Tingatinga, Helbadau, Nholi, Masange, loo maji yard na sepuka
13.Upimaji wingi w amaji umefanyika katika vituo 4 vya mtoni ambavyo ni Hainu-quamquam,Magara-Datlaa, Tsoray na Qamey kwa lengo la usanifu wa mradi wwa maji
14.Ujenzi wa ofisi unaendelea na umefikia 80% ya utekelezaji wake chini ya Mkandarasi Ndika EngineersLtd na wasimamizi wa ndani. Ujenzi uku katika hatua ya umaliziaji
15.Utafiti wa awali kwa ajili ya ukarabati wa mabwawa umefanyika katika wilaya ya kiteto ambapo maeneo matano yameainishwa kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina na kuandaa gharama za ujezi
16.Uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji umefanyika katika mabwawa ya Songwa na Nhumbu wilayani kishapu ambapo ujenzi wa matanki matatu(3) ya kuhifadhia maji na utengenezaji wa mabango 30 ya makatazo ya shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi wa vyanzo vya maji zimefanyika
17.Uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji umefanyika katika kijiji cha Migombani, katika vyanzo vya chemchemi za Abdulu, Mzava, Njoro ya Gunda, Nyaturu na Mto Simba. Ambapo nguzo za mipaka ya kudumu(beacons) 150 zilifyatuliwa na kusimikwa.
18.Uhifadhi wa chanzo cha maji Chemchemi za Qang'dend umefanyika kwa kujengwa bwawa la pili la kuhifadhia mchanga ili kuzuia mafuriko kutoka korongo la mandadaw
19.Usimamizi wa uchimbaji wa visima virefu umefanyika katika vijiji 6 vya Mkalama, Babati, Iramba, Singida na manyoni
20.Utatuzi wa Migogoro miwili(2) iliyopokelewa na kusajiliwa kwenye daftari la migogoro. Migogoro hiyo imetatuliwa(Mgogoro kati ya kijiji cha Balangdalalu na Bwana Laurent Deemay, Mgogoro kati ya viongozi wa Jumuiya ya watumia maji bonde dogo la mto wa Mbu)