Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Habari

HAFLA YA UZINDUZI WA JUMUIYA YA WATUMIA MAJI BONDE DOGO LA ENGARUKA


Tarehe 10/03/2023
HAFLA YA UZINDUZI WA JUMUIYA YA WATUMIA MAJI BONDE DOGO LA ENGARUKA YAFANYIKA
Katika Hafla hiyo iliyohudhuwiwa na Muheshimiwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa wilaya ya Monduli, Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Monduli, Mheshimiwa Diwani, Mtendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji, Wataalam wa Halmashauri ta Wilaya ya Monduli, RUWASA na Bodi ya Maji Bonde la Kati, Wawakilishi wa Taasisi za Kiserikali na zisizo za kiserikali, Viongozi wa Dini, Viongozi wa mila, Wanajumuiya na Waandishi wa habari

Lengo la Hafla hiyo ilikuwa ni kuzindua jumuiya ya watumia maji Bonde dogo la Engaruka

Katika Hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la kati Eng Mwita Chacha amesema kuwa Bonde la kati atatoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha jumuiya ya watumia maji Bonde dogo La Engaruka linatunza na Kusimamia Rasilimali za Maji Kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo pia Mheshimiwa Mgeni Rasmi Ndg Joshua Nassari ameahidi kutoa ushirikiani wa kutosha ili vyanzo vya maji viweze kuwa endelevu pia ameahidi kutoa ushirikiano wote unaohitajika ili kuwezesha jumuiya yetu kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na utaratibu waliojiwekea pia Ndg Joshua Nassari akagusia juu ya hali ya mabadiliko ya tabia nchi jinsi hali ya joto inavyozidi kuongezeka na kusema kuwa ni kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanyika na kusema kuwa tukiharibu mazingira tutawaachia nini watoto wetu hivyo akasisitiza sana kutumia rasilimali zetu za maji vizuri kwa sababu maji hayana mbadala