Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Maji

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Bodi ya Maji Bonde la Kati

Habari

BODI YA MAJI BONDE LA KATI YAFANYA UCHUNGUZI WA BATHYMETRIC


Baada ya ukarabati uliofanyika katika Bwawa la Nanja lililopasuka kutokana na mvua nyingi zilizokuwa zinaendelea kunyesha, Bodi ya Maji Bonde la Kati iliendelea kufanya Bathymetric survey/study ili kujua kina cha maji, ujazo/kiasi cha maji kilichopo na kutengeneza ramani inayoonyesha uhalisia wa chini ya maji. Utafiti huu utasaidia katika usanifu wa kina wa Bwawa unaotarajiwa kufanyika kwa lengo la ukarabati mkubwa, ujenzi wa kidaka maji( intake structure)  pamoja na birika la kunyweshea mifugo maji  (cattle trough) ili kuhakikisha jamii na wakazi wanaozunguka bwawa hilo wanaendelea kupata huduma ya maji  kwa shughuli mbali mbali za kijamii.