Habari
BODI YA MAJI BONDE LA KATI YABADILISHANA UZOEFU NA CHUO KIKUU CHA NELSON MANDELA KILICHOPO MKOANI ARUSHA KATIKA UTAFITI WA MAJI CHINI YA ARDHI

Bodi ya Maji Bonde la Kati imepata furusa ya kutembelewa na Wanafunzi wa Shahada ya Uzamili Katika rasimali za Maji kutoka Chuo Kikuu cha Nelson Mandela kilichopo Mkoani Arusha. Dhamira ya ziara hiyo ni kuona ni namna gani wataalamu wa maji chini ardhi wanaweza kuainisha Maeneo yenye hazina kubwa ya maji chini ya ardhi kwa ajili ya kuchimba visima virefu.Wanafunzi hao wamevutiwa na kazi zilizofanywa na wataalamu wa Bodi ya Maji Bonde la Kati Wilayani Hanang katika kipindi cha Maafa ya Mafuriko..Aidha wanafunzi hao wameishukuru Bodi ya Maji Bonde la Kati kwa kuendelea kutafuta na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa ajili ya vizazi vilivyopo na vijazo