NAIBU WAZIRI WA MAJI AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI SINGIDA

Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) Naibu Waziri wa Maji amefanya Ziara ya Kikazi Mkoani Singida.
Katika Ziara yake Mkoani Singida amefanya kikao kazi na Menejimenti za Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Maji ambazo ni Bodi ya Maji Bonde la Kati, Maabara ya Ubora wa Maji, Chuo cha Maji, RUWASA, SUWASA, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kiomboi(KIUWASA) na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira(MAUWASA).
Katika kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati Mhe. Mhandisi Kundo Andrea Mathew (Mb) Naibu Waziri wa Maji amempongeza Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati Mhandisi Danford Samson wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji ambapo amempongeza kwa kuongeza idadi ya Watumia Maji waliopo katika jiografia ya Bonde la kati na kufanya makusanyo kuongezeka kutoka shilingi milioni 380 hadi kufikia bilioni 1.2 kwa mwaka.