Mgeni Rasmi Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg. Amiri Mkalipa Akihutubia katika Uundaji wa Kamati ya Kidaka Maji Mto Ngarenanyuki.
Mgeni Rasmi Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg. Amiri Mkalipa Akihutubia katika Uundaji wa Kamati ya Kidaka Maji Mto Ngarenanyuki.
Mhe. Amiri Mkalipa amesema kuwa ni jukumu la kila mmoja kutunza vyanzo vya maji, kwani Watumia Maji Wanaongezeka lakini vyanzo haviongezeki hivyo, ameiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Arumeru kushirikiana na Bodi ya Maji Bonde la Kati kufanya ziara ya ukaguzi kuanzia mwanzo wa chanzo cha Mto Ngarenanyuki hadi Mwisho wa chanzo ili chanzo cha Mto Ngarenanyuki kiendelee kuwa salama.
Vilevile, amewataka Wadau wote kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura pamoja na kushiriki Uchaguzi wa serikali za mitaa.