Habari
HAFLA YA UZINDUZI WA JUMUIYA YA WATUMIA MAJI BWAWA LA MWAMAPULI

Uhifadhi wa vyanzo vya maji ni jukumu letu sote.
Tuko tayari kusimamia, kutunza, kuboresha, kutumia na kuendeleza rasilimali za maji ambazo tunazo katika maeneo yetu ndio ilikuwa kauli mbiu katika uzinduzi wa jumuiya ya mwamapuli
Mkurugenzi wa bonde mhandisi DANFORD SAMSON akisema kuwa jumuiya za maji tunaziunda kulinganana na sheria za rasilimali za maji ya mwaka 2009 namba 11 na imefanyiwa marekebisho yake sasa hivi inajulikana kama sheria namba nane ya usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji na maboresho yake ya mwaka 2022
Akiendelea kusema katika usimamizi wa rasilimali za maji kuna ngazi tano ngazi ya juu ni ngazi ya kitaifa, ngazi ya bonde, ngazi ya vitakamaji, ngazi ya vitakio maji na ngazi ya jamii . katika ngazi ya jamii ndo tunapata jumuiya za watumia maji
Akiendelea kusema jumuiya za watumia maji tunaziunda kwa lengo la kusaidia kusimamia rasilimali za maji katika maeneo yetu hasa katika jamii pia jumuiya hizi tunaziunda kwa kutekeleza sera ya maji ya taifa ya mwaka 2002 na sheria yake ya mwaka 2006 sera hii ya maji inasema jumuiya hizi tunaziunda ili zisaidie na tushirikiane kwa pamoja katika swala zima la kuhifadhi vyanzo vya maji ambavyo viko katika maeneo yetu
Akiendelea kusema kwamba bodi ya maji bonde la kati linathamini michango mikubwa yajumuiya kwani jumuiya hizi zimesaidia sana kupunguza vitendo vya uharibifu, ubora wa maji na upatikanaji wake aidha jumuiya zimesaidia kupunguza migogoro ya matumizi ya maji na kupungua kwa vitendo vya uchafuzi
Ukataji wa miti hovyo shuguli za kilimo karibu na vyanzo vya maji, unyweshaji mifugo ndani ya maeneo ya vyanzo vya maji zimechangia kuongeza kwa uharibifu wa vyanzo vya maji.Jumuiya za watumia maji zinaundwa kwa lengo la kusaidia shuhuli za usimamizi wa rasilimali za maji kwa kushirikiana na jamii kwa ukaribu Zaidi
Akiendelea kusema uundaji wa jumuiya zitasaidia kutatua na kujadili changamoto mbalimbali za usimamizi wa rasilimali za maji na kuzitatua na zile ambazo watashindwa kuzitatua zitafikishwa bonde ili kuzitatua ili kuhakikisha maji yanabaki salama
Pia mwisho akawatakia wanajumuiya utekelezaji mwema wa majukumu na mungu awatangulie katika kutunza na kulinda vyanzo vya maji
MHESHIMIWA MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA IGUNGA MHE. SAUDA MTONDOO pia akahutubia akasema uwepo wa bwawa la mwamapoli umekuwa ni kichocheo kikubwa cha maendeleo yetu ya wilaya ya igunga na ni moyo wa wilaya ya igunga. Mchakato wa uundaji wa jumuiya ya mwamapoli ulianza okitoba 16 katika mchakato huo mikutano ilifanyika katika vijiji, vitongoji na wakilishi katika kila kitongoji na kijiji walipewa mafunzo ya kusimamia rasilimali za maji. Vijiji vinavyohusika ni nguvu moja, ikungulya, mwashomwa ambapo chanzo kikubwa cha maji katika maeneo hayo ni bwawa la mwamapoli.pia wawakilishi walitengeneza sheria zitakazo wasaidia kuhifadhi rasilimali za maji
Pia MHE aliwaomba wanaigunga kutunza rasilimali za maji kwani maji ni uhai na ndio tegemeo letu katika ustawi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii
Jumuiya hii imeandaa mpango kazi wa miaka mitatu utakao wawezesha kutatua changamoto mbalimbali walizo ziainisha wakati wa mafunzo
Pia MHE akasema changamoto kubwa tunayonayo katika sekta ya maji ni upatikanaji wa wa maji ya kutosha kukidhi mahitaji kwa matumizi mbalimbali. Vyanzo vya maji nchini vinaendelea kukauka na vingine kupungua maji na hata ubora wa maji umekuwa ni wa mashaka. Shuguli za kibinadamu zinazo fanyika katika katika vyanzo vya maji na kwenye maeneo ya vidakio vya maji vimekuwa vikichangia kwa kiasi kikubwa katika kuharibu na kuchafua vyanzo hivyo miongoni mwa shughuli hizo ni kilimo katika mito na mabwawa. Utaratibu huo umekuwa ni chanzo cha uharibifu wa vyanzo vya maji,miongoni mwa shughuli hizo ni kilimo kando kando ya mito, mabwawa na vyanzo vingine .utaratibu huo umekuwa ni chanzo cha uharibifu wa vyanzo vya maji, shughuli za kibinadamu zinazofanyika pasipokuzingatia sheria ya usimamizi wa mazingira namba 20 ya mwaka 2004 inayokataza shughuli za kibinadamu kufanyika ndani ya mita 60 kutoka kwenye ukingo wa vyanzo vya maji ikiwemo mito, maziwa, mabwawa na vyanzo vingine. Ufugaji na malisho ya mifugo usiozingatia utaratibu umekuwa ukisababisha mmomonyoko wa arthi na ongezeko la udongo katika vyanzo vya maji na hivyo kuongezeka kwa garama za uzalishaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, tabia ya kukata na kuchoma miti hovyo ambayo imekithiri katika maeneo mengi nchini na hivyo kuathiri vyanzo vya maji na kusababisha vyanzo hivyo kukauka
Pia akasisitiza ukifadhi wa vyanzo vya maji kwa vile unahusiana moja kwa moja na uhai usalama na utulivu wa kila kiumbe
Pia akatoa wito kwa viongozi wa kata na vijiji na vitongoji kushirikiana kwa ukaribu sana na jumuiya ambayo inaenda kuundwa na kuzindua la bwawa la mwamapoli
Pia akatoa rai kwa wanajumuiya kwenda kufanya kazi kwa weledi na uadilifu wa hali ya juu